FAMILIA YA RAYUU WAJA JUU KWA PICHA ZA UTUPU ZA MWANADADA RAYUU.




Msanii anayefanya vizuri kwenye  filamu na tamthilia Rayuuamesema kuwa kitendo cha yeye kunadamwa na skendo chafu za picha za ngono  zimemfanya  atofautiane na familia yake hasa wazazi, huku wakimtaka kuchukua hatua za haraka ili aweze kuachana na tabia hizo ambazo zinaweza kuichafulia jina familia.

Msanii huyo amekuwa akionekana kwenye picha za utupu  ambazo zimekuwa zikimchafulia jina, alisema kuwa zimemfanya hadi kutoelewana na familia yake kwani wanahisi ni muhuni kitu ambacho si kweli.

“Familia yangu imechukia sana kutokana na picha zangu ambazo sijui watu wanazipata wapi, naonekana muhuni mbele ya wazazi wangu wakati siko hivyo, kuna watu wana nia ya kunifanya niwe mbaya mbele ya wazazi wangu na watu wanaonizunguka nashindwa kuelewa wananitafutia nini,” alisema.
Newer Posts Older Posts
© Copyright WCB Daily Published.. Blogger Templates
Back To Top