Diva wa filamu za bongo anayejulikana kama Wema Sepetu amemnusuru msanii mwenzake Kajala Masanja kwenda jela miaka saba baada ya kumlipia faini ya fedha taslimu ya Sh.milioni 13.
Hata hivyo wakati Kajala akiachiwa huru, mumewe Faraja Chambo amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela kutokana na kushindwa kulipa faini ya Sh milioni 213.Mke na mume hao walihukumiwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo baada ya kuwatia hatiani kwa makosa matatuya kula njama, kuuza nyumba iliyopatikana katika mazingira ya rushwa ili kuficha ukweli na kosa la utakatishaji fedha.Mahakama ya Kisutu ilitawaliwa na vituko mbalimbali kwani wakati hukumu ikisomwa, Kajala alikuwa akilia muda wote hali iliyosababisha wasanii wengi waliojaa mahakamani kuangua vilio kwa kububujikwa na machozi kwani hawakuweza kutoa sauti wakihofia kukamatwa kwa kuisumbua mahakama.Hakimu Fimbo alipomaliza kusoma hukumu Kajala alijikuta akikaa chini na kulia kwa huzuni, alitolewa nje kuelekea mahabusu na kuwaacha wasanii wakilia na kupanga jinsi ya kumsaidia aweze kutoka gerezani.
Mama mzazi wa Faraja alitoka mahakamani na kuelekea katika mahakama nyingine ya wazi, alipofika humo aliangua kilio kikubwa kilichovuta watu kumfata kujua kulikoni, mama huyo alivua viatu na kuanza kuwakimbiza wapiga picha walioanza kumpiga picha.
Kuwakimbiza na kuwarushia mkoba wake hakuona kama inatosha aliamua kuokota mawe na kuwatishia kuwaopiga nayo, walifanikiwa kumpiga picha lakini walikuja kuondolewa na askari kwa ajili ya utulivu.Wasanii walianza kuchanga fedha kwa ajili ya kulipa faini ya jumla ya Sh milioni 13 lakini Wema aliwakataza na kuwaambia kwamba fedha zote atazilipa, aliondoka eneo hilo kuelekea benki na baada ya masaa mawili alirudi na fedha hizo.
Akisoma hukumu, Hakimu Fimbo alisema upande wa amshtaka katika kesi hiyo ulikuwa na mashahidi saba na waliweza kuthibitisha katika ushahidi wao kwamba washtakiwa walitenda makosa hayo huku wakijua.
"Kuna makosa matatu, kosa la kwanza wanadaiwa Aprili, 2010 walikula njama ya kuuza nyumba iliyokuwa Kunduchi Sala sala jijini Dar es Salaam, Shtaka la pili kuuza nyumba hiyo Aprili 14, 2010 kwa Emiliana Rwegangira huku wakijua kuna notisi inayowakata kufanya hivyo na shtaka la tatu la kutakatisha fedha.
"Ili mahakama itoe uamuzi kwa kosa la kula njama lazima iangalie kosa la pili la kuuza nyumba iliyozuiliwa kuuzwa kwa sababu ilipatikana katika kwa nia ya rushwa, kwa kuangalia ushahidi mahakama inawatia hatiani kwa kosa la pili,"alisema Fimbo.Alisema kwa kuwa shtaka la pili wametiwa hatiani, mahakama inawatia hatiani kwa shtaka la kulanjama kwani limethibitika. Katika shataka la tatu la kutakatisha fedha, mahakama inamtia hatiani mshtakiwa Faraja na kumwachia huru Faraja kwa sababu alihusika katika kuuza nyumba lakini hajui fedha za kujenga nyumba
hiyo zilipatikanaje."Kwa kosa la kwanza la kula njama, mahakama inawatia hatiani washtakiwa wote na watalipa faini ya Sh milioni 5 au kwenda jela miaka miwili kama watashindwa kulipa, Shtaka la pili washtakiwa wote watakwenda jela miaka mitano kama watashindwa kulipa faini ya Sh milioni 8 na shtaka la tatu faraja anatakiwa kwenda jela miaka mitano akishindwa kulipa faini ya Sh milioni 200,"alisema.
Baada ya kutoa adhabu hizo wasanii walihaha kuchangishana lakini Wema aliokoa jahazi kwa kutoa jumla ya Sh milioni 13 kwa ajili ya kumuokoa Kajala ambaye baada ya saa tatu alifanikiwa kutoa kuelekea nyumbani.Kajala aliondoka na gari la kifahari eneo la Mahakama ya Kisutu kwa kulakiwa na ndugu, jamaa na marafiki waliokuwepo eneo hilo.Kajala na mumewe walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza, Machi 15, mwaka jana na kusomewa mashitaka matatu ya kula njama, kubadilisha umiliki wa nyumba baada ya kuiuza na kutakatisha fedha haramu, kosa ambalo halina dhamana kisheria.
Washitakiwa hao wanadaiwa kula njama ya kuhamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi, Salasala, Dar es Salaam, kinyume na kifungu cha 34 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.
Pia, wanadaiwa Aprili 14, 2010, walihamisha umiliki wa nyumba kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.Kajala na mumewe wanadaiwa katika shitaka la tatu kuwa, Aprili 14, 2010, wakijua kuwa ni kinyume na sheria, walifanya kosa la kutakatisha fedha haramu.
Kajala na mumewe wanadaiwa katika shitaka la tatu kuwa, Aprili 14, 2010, wakijua kuwa ni kinyume na sheria, walifanya kosa la kutakatisha fedha haramu.
"Hakuna ubishi kwamba washtakiwa walikaa wakaamua kuuza nyumba, kinachotakiwa kuangalia kama kweli walifanya hivyo kihalali au la kwani ushahidi ulionyesha washtakiwa wote walishiriki katika utaratibu wa kuuza nyumba hiyo.