Anne Makinda apigilia msumari wa mwisho jeneza la Waziri mkuu Mizengo Pinda Taarifa kamili Iko hapa.



Kufuatia ombi la mheshimiwa Mnyika kwa Spika Ana Makinda leo asubuhi bungeni, Ana Makinda amejibu kuwa mpaka sasa hakuna kesi yoyote iliyofunguliwa inayohusu kusimamisha ripoti ya CAG na TAKUKURU isisomwe bungeni, akishangiliwa kwa kelele na vifijo Makinda amesema kuwa hata zile kesi 10 zilizokuwazinasemwa kuhusu IPTL hazipo hivyo ripoti itasomwa kama ilivyopangwa kesho Jumatano.

Itakumbukwa kuwa wiki iliyopita Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliropoka bungeni kuwa yeye amesoma sheria hivyo anashauri busara itumike ili suala hili lisijadiliwe kwa kuwa kuna kesi mahakamani.
Newer Posts Older Posts
© Copyright WCB Daily Published.. Blogger Templates
Back To Top