Leo kutoka kwenye kituo cha Redio cha Clouds Fm wameripoti juu ya tukio la Mwanaume mmoja alipotea kwenye mazingira ya Utata taarifa hiyo imeandikwa kupitia Website ya millardayo.om
Hekaheka ya leo December 11 inatoka Tanga, ambapo jamaa mmoja mwenyeji wa Tabora alikwenda huko kwa lengo la kuoa na baada ya kuoa akakutana na mauzauza ya ajabu hali iliyomfanya mpaka sasa hali yake kiafya kuwa sio nzuri.
Bwana huyo amesema siku ya Jumapili alikwenda nyumbani kwa wakwe zake kuaga lakini akiwa njini kurudi alikutana na msichana mdogo akitokea mbele yake lakini kadri walivyokuwa wakikaribiana msichana huyo alizidi kuwa mrefu, akataka kugeuka kukimbia ambapo akakuta kuna watu wengine wawili nyuma yake ambao walimwagia maji akapoteza fahamu.
Baada ya kuzinduka alijikuta amewekwa sehemu huku waliomzunguka wakijadiliana kumkata ulimi na wengine wakipingana na mawazo hayo, baadaye walimpeleka kwenye mti na kumlazimisha ale nyama ambayo hakujua ni nyama ya nini kisha wakampeleka baharini ambako kulikuwa kumewekwa sherehe nako walitaka kumkata ulimi pia akakataa ambapo kati ya watu hao wapo waliokuwa wakikataa pia kumkata ulimi.
Alifanikiwa kuwasiliana na ndugu zake kwa njia ya message mpaka wakafika mahali ambapo watu hao walimuacha, anasema kwamba anawatambua watu wote waliokuwa wakimfanyia mauzauza hayo japo amegoma kuwataja kwa mke wake.
Nimekuwekea hapa Hekaheka hiyo, unaweza kuisikilliza sasa.