Super Staa Wema Sepetu leo anapandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar kujibu kesi ya kuwashambulia vijana wawili abao majina yao ni Rashid Balazi pamoja na Juma Bushiri
Kama utakuwa mfuatiliaji mzuri wa vyombo vya habari utakuwa ilisikia habari za vijana wawili waliopata kipigo cha mbwa mwizi kwenye nyumba ya staa huyo ambapo mpamba wake Petit Man anadaiwa kuhusika kuandaa mchezo mchafu wa kuwateka na kuwashushia kipigo Rashid pamoja na mwenzake Juma
Ambapo chanzo cha Vijana hao kupata kipigo ni baada ya Petit Man kupoteza simu yake na kuwahisi vijana hao ndio waliochukua simu yake, siku ya tukio vijana hao walikuja katika nyumba hiyo kwa ajili ya kufanya ukarabari wa mabomba ya maji katika nyumba ya staa huyo
Baada ya Petit Man kufanya uchunguzi wake alishirikiana na Wema Sepetu kuwaita vijana wa kazi maarufu kama ‘mbwa mwitu’ kisha kuwapa kipondo ili watoe simu hiyo lakini hadi dakika za mwisho walikataa kuwa jibu lao lilikuwa moja kuwa hakuchukua simu hiyo, baada kupata kipigo vijana hao walikimbilia Kituo cha Polisi cha Kijitonyama jalada la kesi namba KJN/RB/11250/2014 na KJN/RB/11220/2014 ikiwa na kesi ya SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI.
Hata hivyo Wema na Petit walikamatwa na kuachiwa kwa dhamana kisha walisafiri nje ya nchi.
Hivi ndivyo kijana alivyojeruhiwa na kundi hilo la mbwa mwitu
Credit GPL