Mchezaji wa Azam Fc Mrisho Ngassa ameingia tena kwenye headlines baada ya mali zake anazomiliki kuzitaja hadharani akiwa anamiliki nyumba tano, tatu zipo Mwanza na mbili Dar es Salaam na magari nane, benk anakiasi cha zaidi ya Sh. Milioni 20, licha ya mali alizonazo pia anafanya biashara ya usafirishaji na kilimo
Mrisho Ngassa akiwa na watoto wake wawili
Mchezaji huyo anazidi kufunguka kuhusu utajiri alionao
“Katika gari zangu nane, gari tatu za biashara, mbili ni zangu mwenyewe za kutumia, moja ya shughuli za nyumbani wakati wote na mbili nimewagawia baba na mama kila mmoja na yake,”.
“Mimi ujuzi wangu ni soka. Baada ya hapa sitegemei kurudi shule kusomea chochote, nitafanya biashara. Nimekwishaanza kufanya utafiti wa biashara za kufanya,”.
“Sitarajii kufanya biashara za kibishoo za kuigana igana sijui kufungua saluni au maduka ya nguo. Mimi nitafanya biashara kubwa na siku moja nitatatambulika kama mwanasoka wa zamani na mfanyabiashara mkubwa, tayari nina mashamba kama matatu, hapo nazungumzia kilimo, ambacho kwa sasa ni
biashara kubwa,”
Credit Bin Zubeiry