IPTL Waondoa Pingamizi la Bunge Kujadili Escrow, Mahakama yaitaka Ilipe Fidia.

sakata la IPTL


Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imejiondoa katika kesi ya kikatiba iliyoifungua Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kupinga utekelezaji wa maazimio nane yaliyopitishwa na Bunge baada ya kushindwa kupinga mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa serikali. 

Mbali na IPTL kampuni nyingine zilizohusika kupinga maazimio hayo ni Pan Africa Power Solution Ltd (PAP) mmiliki wa IPTL, Habinder Sethi na mmiliki wa kamapuni VIP Engineering and Marketing Ltd, James Rugemalira. 

Mbele ya Jaji Stella Mugasha, wakili wa upande wa utetezi, Gabriel Munyele, akisaidiana na wakili Joseph Sungwa, aliiambia mahakama kuwa hakuna haja ya kuendelea kusikiliza kesi hiyo kwani zuio la muda waliloomba lilikuwa limeshaanza kutekelezwa na Bunge. 

Kufuatia hali hiyo Jaji Mugasha aliitaka kampuni ya IPTL iwajibike kwa kulipa gharama za kesi kwa kushindwa kujiondoa mapema kupinga maazimio hayo, huku wakijua fika yalishaanza kutekelezwa.


Credit Dar24
Newer Posts Older Posts
© Copyright WCB Daily Published.. Blogger Templates
Back To Top